Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa Dhidi ya DR Congo Kufuzu AFCON 2025

Kocha wa Taifa Stars, Hemed Morocco, ameweka wazi kuwa ana imani kubwa na kikosi alichochagua kwa ajili ya mtanange mgumu dhidi ya DR Congo.

Kikosi hiki kinachanganya vijana wenye njaa ya mafanikio na wachezaji wenye uzoefu wa kimataifa, kinaonekana kuwa na uwezo wa kuiletea nchi furaha.

“Nimefurahishwa sana na ubora wa wachezaji walioitwa.

Ni kikosi chenye ushindani mkubwa katika kila nafasi, na ninaamini watatufanya Watanzania tuwe na sababu ya kutabasamu,” alisema Morocco.

Kurudi kwa Mbwana Samatta katika kikosi cha Taifa Stars ni habari njema kwa mashabiki wa soka nchini.

Samatta ambaye amekuwa na msimu mzuri Ugiriki, anatarajiwa kuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika safu ya ushambuliaji.

“Tunatarajia mchezo mgumu dhidi ya DR Congo, lakini tumejiandaa vizuri. Tutapambana kwa nguvu zetu zote ili kuletea nchi ushindi,” alisema Samatta.

Kikosi cha Taifa Stars Kilichoitwa Dhidi ya DR Congo Kufuzu AFCON 2025

Makipa:

  • Ally Salim (Simba)
  • Zuberi Foba (Azam FC)
  • Yona Amos (Pamba)

Mabeki:

  • Mohammed Hussein (Simba)
  • Lusajo Mwaikenda (Azam)
  • Pascal Masindo (Azam)
  • Ibrahim Hamad (Yanga)
  • Dickson Job (Yanga)
  • Bakari Mwamnyeto (Yanga)
  • Abdulrazack Hamza (Simba)
  • Haji Mnoga (Salford City, England)

Viungo:

  • Adolf Mtasingwa (Azam)
  • Habib Khalid (Singida Black Stars)
  • Himid Mao (Talaal El Geish, Misri)
  • Mudathir Yahya (Yanga)
  • Feisal Salum (Yanga)
  • Seleman Mwalim (Fountain Gate)
  • Kibu Denis (Simba)
  • Nasoro Saadun (Azam)
  • Abdullah Said (KMC)

Washambuliaji:

  • Cyprian Kachwele (Vancouver Whitecaps, Canada)
  • Celement Mzize (Yanga)
  • Mbwana Samatta (PAOK, Ugiriki)

Leave a Comment